Tuesday, June 3, 2014

MAMBO YANAYOSABABISHA LUGHA KUTOKUKUA.

Kuna sababu ambazo hupelekea lugha yoyote ile kuto kukua na wakati mwingine ile lugha huweza kufa kabisa. Sababu hizo ni hizi zifuatazo:
Uhaba wa vitabu vya kufundishia, Ni sababu moja wapo ambayo hufanya lugha kuto kuendelea yani kutotumika katika elimu. Kutokana na sababu kwamba ili luhga iweze kukua inatakiwa itumike katika utolewaji wa elimu mbalimbali sasa kutokana na huu uhaba wa vitatu vya kutolea elimu inapelekea ile lugha kufa kwani inakuwa haitumiki katika masuala ya ufundishaji na vitabu kuto kutosheleza kwa kazi hiyo.

 FURAHA SANGA.

Uhaba wa Wataalamu, Lugha huweza kufa pale tu inapokosa watu muhimu wa kuindeleza. Wataalam wa lugha ndio wanaosababisha lugha kuendelea kukua na kutumika kwani wao ndio watu wa muhimu wa kusoma makala mbalimbali, vitabu mbalimbali ili tu kuendeleza lugha  husika. Kwakufanya hivyo lugha huweza  kupata misamiati mingi kutoka lugha nyingine hivyo kupelekea lugha kukua kutokana na hawa wataalam. Hivyo ni watu wa muhim katika suala zima la uenezaji wa luhga ili isiweze kufa.


Suala la Kasumba, Ni sababu ambayo hupelekea lugha kufa. Kasumba hii ni pale tu mtu anapoona lugha fulani ni bora zaidi kuliko nyingine basi ile ambayo huonekana sio bora  hufa. Watu huamini kuwa lugha ya Kiingeleza ni bora zaidi kuliko luhga ya Kiswahili na hii pia inafanya watu kuona mtu akizungumza kiingeleza  ndio msomi au anajua zaidi lugha kitu ambacho sio kweli, hivyo basi ile lugha ambayo haijathaminiwa huweza kufa.

Sera ya Lugha, Lugha ya Kiswahili hutumika kufundishia elimu ya msingi lakini sekondari na vyuo hutumika lugha ya kiingileza. Kutokana na sera ya luhga  ya nchi yetu kusababisha lugha ya kiswahili kufa kwasababu inakuwa haitumiki kwa mkazo kwani huwa kama somo tu wala sio luhga ya kutolea elimu kama ilivyo katika elimu ya msingi.

Kuwepo kwa wanyama wakali, Kuna wanyama  wakali ambao walisababisha lugha ya kiswahili kuto kukua. Mfano simba katika misitu ya tsavo kitu ambacho kilipelekea watu kuogopa kupita katika misitu hiyo na kwenda sehem nyingine kuendeleza lugha.

Makabila shupavu, Kulikuwa na makabila ambayo ni shupavu kwani hawakuruhusu misafala ya watumwa kuweza kupita katika maeneo yao. Mfano kabila la maasai wao hawakuruhusu misafala hii hivyo kusababisha lugha ya kiswahili kuto kufika katika maeneo yao.


 

Monday, June 2, 2014

MAMBO YANAYO SAIDIA LUGHA KUKUA

Kuna mambo mbalimbali anayosaidia lugha yetu kukua.

Kutumika katika elimu, Suala hili la elim husaidia lugha yetu kukua na kuendelea kutumika bila kufa. Kupitia utoaji wa elim mbalimbali kwa lugha hii ya Kiswahili ndio sababu ya kukua kwakekwani elim hiyo huanzia shule za msingi ikiwa ndio lugha ambayo hutumika kutolea elim, sekondari huwa ni somo ambalo hufundishwa na vyuo huwa kozi ambayo mtu husomea kwa miaka mitatu.Uundaji wa vyombo mbalimbali ambavyo husaidia katika ukuaji wa lugha yetu, Kuna BAKITA(Balaza la Kiswahili Tanzania) TUKI(Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili) BAMITA(Balaza la Mitiani la Taifa). Hivi ni baadhi ya vyombo ambavyo husaidia katika suala zima la ukuzaji wa lugha yetu ya Kiswahili.

Uwepo wa vyombo vya habari, Vyombo hivi vya habari husaidia sana katika suala zima la ukuzji wa lugha yetu kwasababu lugha ambayohutolewa huwa ni ya kiswahili hivyo kufanya watu wengi kuelewa ujumbe ambao unatolewa. Mfano kuna redio, televisheni na magazeti. Hivi ni baadhi ya vyombo ambavyo husaidia katika ukuzaji na uendelezaji wa lugha ya kiswahili.

Suala la Dini, Pia dini inaidia katika uenezaji wa lugha ya kiswahili kwani mahubili hutolewa kwa lugha hii ya kiswahili ambayo hufanya watu kuelewa ujumbe ambao unatolewa. Wakati wa ukoloni pia dini ilisaidia kukuza ligha na kufanya iendelee hadi leo.

Suala la biashara, Pia biashara nayo imesaidia sana katika ukuzaji wa lugha hii ya kiswahili. Biashara ambazo zinafanyika huendeshwa kwa lugha ya kiswahili hivyo hupelekea lugha kukua zaidi. Hata katika kipindi cha wakoloni biashara ilisaidia kukuza lugha ni kwasababu ya luhga iliyokuwa inatumika ni ya kiswahili.

UZINDUZI WA ALBAM YA PILI, ATOSHA KISAVA


Karibuni katika uzinduzi huu, kufika kwako ndio kufanikisha zoezi hili

KARIBUNI, DHANA NA FASILI(MAANA) YA LUGHA

Wapo wataalamu mbalimbali waliojaribu kuifafanua maana ya lugha kwa mfano Mgullu(1999) katika kitabu chake cha Mtalaa wa Isimu akirejelea mawazo na maoni ya wataalamu mbalimbali amejaribu kuifafanua maana ya lugha kama ifuatavyo.


Trudgil,(1974)anasema "Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zinazotumiwa kwa mawasiliano miongoni mwa watu wa jamii fulani yenye utamaduni wake"

Sapir,(1921) anasema "Lugha ni mfumo ambao mwanadamu hujifunza ili autumie kuwasilishia mawazo, maoni na mahitaji. Mfumo huu hutumia ishara ambazo hutolewa kwa hiari"

Weber,(1985) anasema "Lugha ni mfumo wa mawasiliano ya mwanadamu ambao hutumia mpangilio maalumu wa sauti kuunda vipashio vikubwa zaidi kwa mfano mofimu, maneno na sentensi" Pia anadai kuwa lugha ni mfumo wowote wa mawasiliano ya watu kwa mfano lugha ya Kifaransa. lugha ya Kihindi.

Kamusi ya TUKI(1990)inasema,"Lugha ni mfumo wa sauti zinazotumiwa na watu wa jamii fulani wenye utamaduni unaofanana ili kuwasiliana"

Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa lugha ni mfumo wa sauti za nasibu ambazo zimekubaliwa na jamii ya watu fulani ili zitumike katika kukidhi mawasiliano yao ya kila siku katika nyanja mbalimbali za maisha mfano siasa, uchumi na utamaduni. Kutokana na maana mbalimbali za wataalamu hao walionukuliwa na Mgullu(1999) tunapata mambo ya fuatayo yanayounda au yanayopatikana katika lugha yoyote ile kama;

a) lugha ni mfumo wa sauti. Sauti mbalimbali zinazopatikana katika lugha fulani hupangwa kwa namna ambayo sauti hizo huungana pale zinapotamkwa (au kuandikwa) kutoka sehemu mbalimbali katika mfumo wa utamkaji (utazungumziwa katika mada zijazo)

b) lugha ni sauti za mawasiliano: lengo kuu la lugha yoyote ni kukidhi mahitaji ya mwanadamu ambayo ni mawasiliano. Mawasiliano hayo husaidia katika kupanga,kuagiza na kutimiza mambo mbalimbali ya maisha ya kila siku ya mwanadamu.

c) lugha ni sauti za nasibu:Hakuna mwanadamu anayezaliwa akiwa anafahamu lugha bali hukutana nayo kibahati mbaya tu. Hujifunza tu pale anapowasiliana na watu au pale mtu anapozungumza na yeye kusikilza na kuiga mfano mtoto mdogo anapofikia umri wa kuanza kuongea hujifunza kutamka silabi au maneno macache taratibu mwishowe hutamka sentensi nzima. Vile vile dhana ya unasibu katika lugha ni kwamba hakuna mahusiano ya moja kwa moja kati ya kiashiria au kitaja(neno au jina) na kiashiriwa au kitajwa(kile kinachotajwa). Hakuna uhusiano kati ya neno meza na kitu chenyewe ambacho kinaitwa meza.

d) lugha ni sauti za nasibu za kusemwa na watu: binadamu ndiye kiumbe pekee mwenye kutumia lugha, wanyama ndege na viumbe wengine mfano wadudu wao hawana lugha hata kama wanatoa sauti mbalimbali zinazowawezeshs kuwasiliana. Kwa mfano Trudgil(1980) akinukuliwa na Mgullu(1999) anasema sauti za nasibu ambazo hutumika katika mawasiliano ni za wanadamu. Sauti hizi vilevile huweza kuwasilishwa kwa kutumia alama maalumu yaani maandishi ingaw pia chaweza kuwa kigezo dhaifu sana kubainisha unasibu wa lugha ya mwanadamu kwani alama hizo pia huashiria sauti za kusemwa na watu.

e) lugha kama chombo cha utamaduni fulani: kila lugha ina utamaduni wake. Lugha yoyote ile hutumikia utamaduni wa watu fulani hivyo basi hakuna lugha bora duniani kuliko lugha nyingine kwa mfano lugha ya Kiingereza si bora duniani kuliko Kichina , Kihispania, Kijerumani au Kiswahili hata kama Kiingereza kinatumika kila kona ya dunia hasa kwa shughuli za kimataifa ikiwa lugha hii ilisambazwa na Waingereza kipindi cha ukoloni sehemu mbalimbali duniani.

f) lugha ni njia ya mawasiliano: lugha yoyote ile lengo lake kuu ni kukidhi haja ya mawasiliano kati ya mtu na mtu au mtu na kundi au watu na watu. Hivyo kama lugha haikidhi mawasiliano haina maana.

FAIDA ZA LUGHA


Kulingana na maelezo hapo juu lugha ina faida nyingi kama ifuatavyo:
Chombo cha mawasiliano miongoni mwa watu

Chombo cha kukuza utamaduni wa jamii fulani kwani lugha yoyote lazima iwe na utamaduni wake kulingana na jamii ya watu husika mfano naman ya kutumia lugha kw akusalimiana
Inaunganisha watu, lugha huunganisha watu wa jamii na mataifa mbalimbali kupitia ukalimani na utafsiri
Kitambulisho
lugha pia huweza kuwa kama kitambulisho cha utaifa au kabila mfano Mtanzania anayezungumza Kiswahili akiwa ughaibuni nje ya nchi yake na kukutana na mtu kutoka Tanzania anayejua kiswahili atafamika mapema pindi atakapozungumza.
]Lugha ina uwezo wa kukuza fasihi ya jamii husika iwe kwa njia ya maandishi au mazungumzo.

HASARA ZA LUGHA.

 >Hasara kuu ya lugha ni utengano. Jamii huweza kutengana kwa kukosa mawasiliano pindi wakutanapo watu wasiofahamu lugh kila mmoja lugha ya mwenzake huwa kama bubu japo kwa muda mfupi.

MAREJELEO


Mgullu,R.S(1999)Mtalaa wa Isimu,Fonetiki,Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili, Nairobi Kenya, Longhorn Publishers(Ukurasa wa 6 hadi 10)


Chanzo cha habari hii: http://tanzaniaswahili.blogspot.com/2013/01/TUIPENDE LUGHA YETU

Wapenda wangu, nimefungua blogger yangu ambayo itahusika na masuala mbalimbali ya lugha yetu ya Kiswahili hivyo mpendwa wangu naomba ushirikiano wenu. Kwani nia na lengo ni kukuza na kuendeleza lugha yetu ya Kiswahili.
FURAHA SANGA